Jukumu la waajiriwa kuwajibikia hela zilizo chini ya utunzi wao

Waajiriwa wana jukumu  la kuwajibikia hela pamoja na rasilimali nyingine chini ya utunzi wao. Kifungu cha 10 (2) cha KATIBA ya Kenya kinaeleza kuwa vigezo vya maadili mema ya kitaifa pamoja na vigezo  vya utawala bora miongoni mwa vingine ni utawala bora wenyewe, uadilifu, uwazi pamoja na uwajibikaji. Uwajibikaji aghalabu huzingatiwa kama kigezo muhimu katika taratibu za utendakazi za kampuni. Kwa mwajiriwa uwajibikaji unahusu kuwa tayari kujibu na kutoa maelezo kuhusu maswali yoyote yanayoweza kuibuka kutokana na utendakazi wake. Katika kesi ya Nixon Otieno Awuor na wengine 4 dhidi ya inspekta Jenerali wa shirika la kitaifa la polisi na wengine 4 (2008) eKLR . Mahakama ilishikilia kuwa walalamishi hakuweza kuwajibikia na kujibu shutuma  za mwajiri wao kwa mujibu wa kifungu 10 na sura ya 6 ya KATIBA. Mbali na hayo mahakama pia ilielekeza kuwa hakuna mwajiriwa ambaye hawezi kuchukuliwa hatua kazini wala ambaye hawezi kutakiwa na wakubwa wake kuwajibikia maamuzi yake. Hatua za walalamishi za kukataa, kukaidi, na kukiuka wajibu wao kwa mshatakiwa kulitosha kuchukuliwa kuwa hatu ya kumkaidi mwajiri wao suala ambalo lingeweza kutumiwa kama kigezo cha adhabu dhidi yao. Rejelea tovuti: http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/154298/

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s