Uhuru wa Mwajiri kushiriki na shughuli za vikundi vya waajiri

Kwa mujibu wa KATIBA ya Kenya ya mwaka 2010 , mwajiri ana haki ya kushiriki katika shughuli za mashirika ya waajiri. Kifungu cha 41 cha KATIBA ya Kenya ya mwaka 2010 kinaelekeza kuwa kila mwajiri ana uhuru wa kuanzisha na kujiunga na shirika la waajiri. Katika kesi ya muungano wa wafanyikazi wa serikali za kaunti nchini Kenya dhidi ya serikali ya kaunti ya Nyeri na mwingine (2015) eKLR, mahakama ilipendekeza  hatua za usawa katika suala la ufanyikazi kama zilivyoelezewa kwenye kifungu 41(2), (3), (4) na (5). Katika kifungu cha 41(2) kila mfanyikazi ana haki ya kupata ujira ulio sawa na kazi anayoifanya, haki ya mazingira mazuri ya kufanya kazi, haki ya kujiunga na kushiriki katika shughuli za miungano ya wafanyikazi na hata kushiriki kwenye migomo. Katika kifungu cha 41(3) kila mwajiri ana haki ya kuanzisha na kujiunga na mashirika ya waajiri na pia kushiriki   katika shughuli na mipangilio ya shirika husika la waajiri.  Rejelea tovuti  http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/116963/v

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s