Haki ya mwajiri kujuzwa mwajiriwa anapoondoka kwenda likizo

Mwajiri ana haki ya kujuzwa punde tu mwajiriwa anapoondoka na kwenda kwenye likizo ya kupata matibabu . Sehemu ya 30(2) ya sheria ya ajira inaeleza kuwa mwajiriwa anaweza tu kuondoka ili kupata likizo ya matibabu baada ya kumjuza ama kusababisha kujuzwa kwa mwajiri kuhusu hali hiyo haraka iwezekanavyo. Katika kesi ya Antony Kanai dhidi ya Cannon Assurance Limited (2008) eKLR   mahakama iligundua kwamba kwa mujibu wa ushaidi mlalamishi alichukua hatua ya kuenda likizoni bila ya ombi lake kuidhinishwa na hivyo kupatikana na hatia ya kukosa kufika kazini bila ruhusa. Mlalamishi huyo pia alitakiwa kuyaacha majukumu yake mikononi mwa msimamizi wake kabla ya kwenda likizoni jambo ambalo hakulitekeleza na hivyo kuchukuliwa kukaidi maagizo ya wakubwa wake kazini. Mahakama ilishikilia kwamba mshtakiwa alikuwa hajakiuka sheria yoyote katika kumpiga kalamu mlalamishi. Rejelea tovuti: http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/161434/

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s