Haki ya mwajiri kumshusha mwajiriwa wake cheo kazini.

Mwajiri ana haki ya kumshusha mwajiriwa cheo kazini. Sheria katika ukawaida wake inaeleza kuwa kuzushwa cheo kwa mwajiriwa na mwajiri kutoka cheo kimoja hadi kingine ambacho kina mshahara wa chini ukilinganishwa na wa nyadhifa aliyokua ameshikilia kuko mikononi mwa mwajiri. Hili linaweza kufanyika iwapo mwandishiwa amepoteza imani kwa mwajiriwa. Katika kesi ya Gerald Okumu Aoko dhidi ya  taasisi ya Kenya Marne na mwingine (2014) eKLR . mlalamishi aliteta kwamba hakuwa amepewa nafasi ya kuweza kujitetea kabla ya kuzusha cheo na kupata uhamisho wa kikazi. Korti ilibaini kuwa hii ilikuwa kesi ya mlalamishi kutaka haki zake kwenye mkataba kuzingatiwa. Mlalamishi hata hivyo alipewa barua ya kuonyesha kuwa alifaa kuchukuliwa hatua na vilele kukawa na kikao katika ofisi ya mkururgenzi  kabla ya kusimamishwa kazi kwa muda na baadaye kuzusha cheo. Mahakama ilishikilia kuwa mwajiri alikuwa na haki ya kumzusha mwajiriwa cheo iwapo alikuwa amekosa Imani kuwa mlalamishi ana uwezo wa kuwasimamia wahasibu wengine. Rejelea tovuti : http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/101877 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s