Jukumu la kuwajuza waajiri kuhusu majeraha katika kazi

Waajiriwa wana jukumu la kuwajuza waajiri wao matukio ya majeraha katika sehemu za kazi. Sehemu ya 21(3) ya sheria ya usalama na afya ya sehemu za kazi, mwajiriwa anapaswa kumjuza mwajiri wake haraka iwezekanavyo kuhusu matukio yoyote ya majeraha katika sehemu za kazi. Hili kwa sababu mwajiri pia ana jukumu la kumjuza mkurugenzi wa masuala ya afya na usalama katika sehemu za kazi  baada ya kupokea ujumbe huo kutoka kwa waajiriwa wake. Katika kesi ya Julius Chacha  Mwita dhidi ya Kampuni ya uchukuzi wa ndege ya Kenya Airways na mwingine (2015) eKLR. Mahakama iliamua ifuatavyo. Mlalamishi kwa kuzingatia sehemu ya 21(3)  ya sheria ya usalama na afya katika sehemu za kazi ambayo inaeleza kuwa iwapo kuna tukio la ajali ambayo haijasababisha maafa katika sehemu za kazi , mwajiri anafaa kutuma ujumbe kwa njia ya maandishi kwa afisa anayesimamia masuala ya afya na usalama ndani ya siku saba tangu kutokea kwa ajali hiyo. Mwajiriwa anatakiwa kupeana taarifa la tukio hilo kwa mwajiri wake kwa njia yam domo.  Katika tukio hili mlalamishi alipiga ripoti kabla hajakimbizwa hospitalini kwa matibabu.Rejelea tovuti:http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/112319

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s