Jukumu la mwajiri kuhakikisha kwamba mwajiri ana makazi

Kwa mujibu wa sheria ya ajira, waajiri wana jukumu la kuhakikisha kwamba waajiriwa wao wana makazi / kutoa  makazi kwa  waajiriwa wao. Sehemu ya 31 ya sheria ya ajira yam waka wa  2007 inaeleza kuwa mwajiri lazima atoe makazi kwa waajiri wake kwa mujibu wa sheria au ahahakikishe kuwa amewalipa marupurupu ya waajiri wake kupata makazi. Kwa mujibu wa sehemu ya 31 mwajiri anathibitiwa na makubaliano kati yake na mwajiriwa wake au makubaliano ya utendakazi katika nyanja hiyo. Katika kesi kati ya Muungano wa kitaifa wa watunza usalama binafsi na kampuni ya usalama ya Kenya Kazi.  Pande hizi mbili zilikuwa zimefeli katika  kupata mwafaka kwenye makubaliano ya pamoja ilivyokuwa imeagizwa mapema na mahakama . kama sehemu ya mukataba wa makubaliano, mwajiri alipaswa kuhakikisha kuwa mwajiriwa waliokuwa wanachama wa miungano wana marupurupu yatakayowawezesha kupata makazi. Mahakama ilishikilia kwamba ni jukumu la mshtakiwa  kuwapa walinzi wake sehemu za makazi bila malipo katika ama karibu na ubalozi wa Marekani ama  vinginevyo wagharamie ada itakayowawezesha waajiriwa hao kupata makazi hayo. Rejelea tovuti:http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/108480

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s