Jukumu la waajiriwa kuifadhi siri za kazini.

Sheria inampa mwajiri haki ya kuwataka waajiriwa wake kuhifadhi siri za kazini. Sheria katika ukawaida wake inaelekeza kuwa katika kipindi cha kawaida cha ajira , mwajiriwa atakuwa amejua siri za kazini za mwajiri wake. Kwa muda amabao siri hizo zitakuwa za manufaa kikazi na ikiwa kulikuwa mna maagano ya kuzihifadhi kama siri, basi mwajiriwa  ana wajibu kisheria  wa kutotoa taarifa hiyo kwa yeyote yule.  Mwajiriwa ana Wajibu huu wa kuhifadhi siri hii hata ingawa awali hakukuwa na maagano ya kuzihifadhi au kifungu kwenye mkataba wa ajira wa mwajiriwa. Wajibu huu kwa kawaida huweza kuendelea hata baada ya kufika kwa kikomo kwa mahusiano ya wawili hawa kikazi. Katika kesi ya: David Makau dhidi ya kampuni za Devson (2019) eKLR.
Katika kesi hii , hata kama mahakama iligundua kuwa kupigwa kalamu kwa mwajiriwa hakukufanywa kwa njia ya haki,  ilikataa kutoa agizo la kufidiwa kwa mwajiriwa kwa sababu alikuwa ameenda kinyume cha kijisehemu kwenye mkataba wake wa ajira  ambapo mlalamishi huyu ambaye alikuwa mhasibu alikuwa amefaulu kupata habari zinazohusu mishahara ya waajiriwa wa mshtakiwa  na katika kipindi hicho cha ajira akawajuza waajiriwa wengine ambazo hawakupaswa kufahamu  taarifa hizo na hawana uhusiano wowote na kesi inayoendelea sasa. Rejelea tovuti :http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/170170/

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s