Wajibu wa mwajiri kuifadhi rekodi za waajiri wake.

Mwajiri ana wajibu wa kuhifadhi rekodi zote za waajiriwa wake. Sehemu ya  74(1) ya sheria ya ajira inaeleza kuwa mwajiri anafaa kuweka hifadhi ya rekodi  ya waajiriwa wake wote ambao ameingia katika mkataba nao chini ya sheria ya ajira. Katika kesi ya Silas Mutwiri dhidi ya Haggai Multi-cargo services limited (2013) eKLR  mahakama ilishikilia kwamba hiyo sehemu ya 74 ya sheria ya ajira  inawataka waajiri wote kuhifadhi rekodi za ajira na kusiwasilisha mahakamani kama ushahidi. Hili si jukumu la mwajiriwa . hili ni jukumu la mwajiri ambaye ana usemi zaidi katika ule uhusiano wa mwajiri na mwajiriwa. Hizi rekodi hazikuwasilishwa kortini kamwe katika kesi hii. Iwapo hilo halikufanyika kwa mujibu wa sehemu ya 20 na 74 ya sheria ya ajira , uamuzi utafanywa kwa faida ya mlalamishi. Katika kesi hii hakukuwa na rekodi kuwa , likizo, kazi inayofanywa katika muda wa ziada, chini ya sehemu ya 35(6) ilikuwepo, na kwa sababu ya hilo madai ya mlalamishi yalichukuliwa kuwa ya kweli. Rejelea tovuti:http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/93212

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s