Mwajiri ana wajibu wa kutoa/kuwasilisha msimamao wake/ wa shirika kuhusu suala la unyanyasaji wa kijinsia.

Sehemu ya 6  ya sheria za ajira inaeleza kuwa mwajiri yeyote ambaye ataajiri zaidi ya waajiriwa ishirini anapaswa kutoa taarifa ya msimamo wa shirika lake kuhusu unyanyasaji wa kijinsia. Taarifa hii itahusu miongoni mwa mambo mengine mikakati ambayo mwajiri anaiona ikiwa bora katika kuzuia matukio ya unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya kazi. Katika kesi ya J W V dhidi ya Securex agencies limited (2018) eKLR. Mahakama ilizingatia sehemu ya 6(2) ya sheria ya uajiri ambayo ilimpa mlalamishi jukumu la kuwasilisha taaraifa ya msimamo na utaratibu kuhusu dhuluma za kijinsia. Kwa mujibu wa sehemu ya 6 (3) taarifa hiyo ilifaa kutoa fasili za maana ya dhuluma za kijinsia kama ilivyo katika sheria, haki ya waajiriwa   kufanya kazi katika mazigira yasiyo na unyanyasaji wa kijinsia, hatua zinazochukuliwa kukinga dhidi ya unyasasaji wa jinsia, ieleze utaratibu wa kupiga ripoti iwapo kisa cha unyanyasaji wa kijinsia kinaweza kutokea, na pia usiri kuhusu suala hilo iwapo kutakuwa na haja ya utfiti kufanyika. Katika kesi hii mahakama ilibaini kuwa mlalamishi alikuwa amedhulumiwa kijinsia kwa mujibu wa maneno ya msimamizi wake wakiwa gwarideni. Mahahkama pia ilibaini kuwa mshtakiwa alitoa  taarifa na utaratibu unaohusu masuala ya dhuluma za kijinsia na kuiweka wazi kwa waajiriwa waake wote kama inavyotakikana kwa mujibu wa sehemu ya 6 (4) ya sheria. Na mshtakiwa kwa mujibu wa maneno ya msimamizi wake wakiwa gwarideni yalimwanika mlalamishi kwa dhuluma za kijinsia  na yalizusha hisia zake za kibinadamu kama ilivyo katika kifungu cha 28. http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/153700/

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s