Waajiri wana haki ya kuajiri kwa mujibu wa utaratibu uliopo wa kitaifa wa kuajiri.

Sehemu ya5 ya sheria ya ajira inaeleza kuwa haitakuwa uonevu kwa upande wa mwajiri iwapo atamwajiri raia yeyote wa Kenya kwa mujibu wa utaratibu uliopo wa ajira. Utaratibu wa kitaifa wa ajira ni maono na mikakati ya kuafikia malengo ya kitaifa katika ajira . Utaratibu wa kitaifa wa ajira ni sharti ukuze utendakazi mwema ambapo vigezo vya kimataifa vyautendakazi, na haki za kimsingi za wafanyikazi zinaenda moja kwa moja na harakati za kuibua nafasi za kazi. Katika kesi ya Koki Muia  na kampuni ya Afrika Mashariki ya Samsung electronics (2005) eKLR katika suala hili mlalamishi alileta dai la kuachishwa kazi kwa njia isiyo ya haki hata hivyo mshatakiwa kwenye jibu lakeakasema kuwa mlalamishi alikuwa hana ujuzi na maarifa ya kutosha kusimamia kitengo alichopewa . Mshtakiwa vilevile alieleza kuwa alimwachisha mlalamishi kazi kwa kuzingatia utaratibu na sheria za ajira. Hata hivyo mahakama ilikinzana na madai ya mshtakiwa na kutamka kuachishwa kazi kwa mlalamishi kuwa kusiko kwa haki na mbako hakukuzingatia sheria. Mahakama ilizingatia sehemu ya 5 ya sheria ya ajira ambayo inafasili utaratibu wa ajira kuwa: “ utaratibu wa ajira au atendaji wa uatartibu huo unahusu lolote linalohusiana na harakati za ajira, utangazaji wa nafasi za ajira pamoja na mbinu zinazotumiwa kuteua wale ambao wameonyesha nia ya kuwania nafasi hizo za ajira, upeanaji wa nafasi hizo za ajira pamoja na utaratibu unaotumika, migao ya kazi, ujira utakaotolewa, manufaa atayopata mwajiriwa , sheria na masharti ya ajira hiyo, mazingira ya kazi na raslimali iliyopo, mafunzo na kuendeleza kwa maarifa, utaratibu wa kutathmini utendakazi, kupandishwa cheo, uhamisho wa kazi, kuzushwa cheo kazini, kuachishwa kazi pamoja na utaratibu wa adhabu itakayotolewa kwa wafanyikazi kwa makosa mbalimbali. http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/112160/

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s