Kila mmoja ana haki ya usawa katika utekelezaji wa kazi yake.

Kwa mujibu wa KATIBA ya Kenya kifungu cha 41, kila mwajiri ana haki ya usawa katika utendakazi wake ikiwemo ile ya kuasisi ama kujiunga na chama cha waajiri na pia kushiriki katika shughuli na mikakati ya chama hicho. Katika kesi ya muungano wa wafanyikazi wa serikali za kaunti na serikali ya kaunti yaNyeri na mwingine (2015) eKLR lilikuwa ni pendekezo la mahakama kuwa vigezo vya haki katika utendakazi  vimewekwa dhahiri kwenye vifungu vya 41(2), (3), (4) na (5) vya KATIBA. Kwa mujibu wa kifungu  cha 41(2)  kila mfanyikazi ana haki ya kupata ujira ulio wa haki, haki ya kuhakikishiwa ana mazingira mema ya kufanya kazi, haki ya kujiunga na kuhusika katika shughuli za vyama vya miungano ya wafanyikazi na vilevile haki ya kugoma. Kwa mujibu wa kifungu cha 41(3)  kila mwajiri ana haki haki ya kuunda au kujiunga  na vyama vya waajiri na kushiriki katika shughuli za vyama hivyo.
Rejelea tovuti: http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/116963/

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s