Mwajiri ana haki ya kuwatenga waajiriwa kufikia baadhi ya vitengo vya ajira .

Sehemu ya 5 ya sheria ya ajira inaeleza kuwa katika hali fulani na kwa sababu ya umuhimu wa usalama wa kitaifa haitakuwa uonevu kwa upande wa mwajiri iwapo atawatenga waajiriwa wake kufikia vitengo fulani vya ajira. Maonevu tangu kale yameweza kupingwa katika sehemu za kazi hata hivyo kuna nyakati ambazo haki hii ya kutotengwa kazini inaweza kukosa kuzingatiwa na baadhi ya waajiriwa wakaondokea kuwa na haki ambazo wenzao hawana.
Katika kesi ya Wycliffe Lisalitsa dhidi ya Afisa mkuu mtendaji wa hospitali ya kitaifa ya Kenyatta na wengine tano (2014) eKLR. Washtakiwa walijibu kwa kusema kuwa walalamishi hawakuwa wanachama wa chama cha kitaifa cha madaktari, wauguzi, na madaktari wa meno nchini Kenya na hivyo hawangeweza kuhusishwa katika majadiliano ya kuongezewa marupurupu ambayo vitengo vyao vya ajira havikufaa kupokea na hakukuwa na uonevu wowote katika utekelezaji wa ulipaji wa marupurupu hayo. Mahakama ilishikilia kwamba walalamishi hawakuweza kuthibitisha kuwa walikuwa wamehusishwa katika mawasiliano ya awali  kwa ajili ya ulipaji wa marupurupu hayo. Rejelea tovuti:http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/99841

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s