Waajiriwa ambao utendakazi wao haujadumu kwa muda wa zaidi ya miezi mitatu hawana haki ya kupatiwa mkataba wa ajira ulioandikwa.

Sehemu ya 9(1a) ya sheria ya ajira inaeleza kuwa mkataba wa ajira utatolewa tu kwa  waajiriwa ambao wamo katika kazi ambayo itachukua muda wa miezi mitatu na Zaidi. Ilivyo kawaida ni kwamba mikataba yote inafaa kuandikwa hata hivyo iwapo mwajiriwa atakuwa kazini kwa muda unaopungua miezi 3, mwajiri ataamua kumpa au kutompa kandarasi yaajira kwa njia ya maandishi. Katika kesi ya Krystalline Salt limited dhidi ya Kwekwe Mwakele na wengine 67 (2017) e KLR Kwa mujibu ya sehemu ya 37 ya sheria ya ajira, mahakama ina uwezo wa kubadililisha vigezo vinavyozingatiwa katika ajira na kuamua kuwa maajiriwa wameajiriwa kwa vigezo vinavyooana na sheria ya ajiara. Katika kesi hii  mlalamishi alitenda kazi kwa siku mfululizo , jumla ya siku alizofanya kazi zilikuwa ni Zaidi ya siku 30 na kwa mujibu wa sehemu ya 37(1) alikuwa ameanza kulindwa na sheria  sehemu ya 35(1) inayomlinda kutokana na kufutwa kazi. Chini ya sehemu ya 31(1) (c) mwajiriwa hawezi akaachishwa kazi bila kupokezwa ilani ya siku 28. Katika muktadha  mlalamishi alizuiliwa na mahakama  kutokana na kuchukua hatua ya kumfuta mshatakiwa bila kumpa ilani ya siku 28 kwa njia ya maandishi.http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/132633/

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s