Haki ya mwajiriwa kujiunga na muungano wa wafanyikazi

Kila mwajiriwa ana haki ya kujiunga na muungano wa wafanyikazi. Kifungu cha 41(2)(c ) cha KATIBA kinatoa hki ya kila mfanyikazi kuasisi ama kujiunga na muungano wa wafanyikazi, imewekwa wazi kuwa kila mfanyikazi ana …” haki ya kuanzisha , kujiunga na kushiriki katika shughuli  na mipangilio ya muungano wa wafanyikazi.” Suala hili ni haki kikazi n ahata kisiasa. Haki ya kuatangamana inawapa watu uwezo wa kuunda miungano ya kisiasa au makundi mengine yoyote watakayopenda , kudumu kwenye miungano hiyo, kuondoka kwenye miungano hiyo, kuondoka kwenye miungano hiyo na kujiunga na mingine na kadhalika, kwa hivyo  mtu hawezi akalazimishwa  kudumu kwenye muungano amabao hawataki kujihusisha nao tena. Hili linahusiana mojakwa moja na haki ya uhuru wa kibinafsi kwa sababu haki hizi pamoja na uhuru vinahusiana. Sheria zinazohusiana na usajili wa miungano hiyo hazifanyi kukataa kusajili makundi hayo bila sababu tosha. Mbali na hayo wanachama wa muungano huo lazima waweze kusikilizwa kabla ya uamuzi kufanywa kuhusu kutosajiliwa kwa kundi hilo. Marejeleo. Tazama kesi kati ya baraza la magavana dhidi ya mwanasheria mkuu na wengine (2017) eKLR inayopatikana katika tovuti: http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/134814/(Dec 2017) mahakama ilieleza kuwa  uhuru wa kutangamana ni wa kimsingi ili kuhakikisha uchaguzi wazi usawa na wa kuaminika.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s