Haki ya mwajiriwa kuvunja mkataba wa majaribio ya utendakazi wake bila ilani yoyote au ilani ya muda mfupi.

Mwajiriwa ana haki ya kuvunja mkataba wa majaribio ya utendakazi wake bila ilani yoyote au kwa ilani ya muda mfupi . Sehemu ya 41 ya sheria ya ajira  inaeleza kuwa  mwajiri kabla ya kumfuta kabisa mwajiriwa wake ampe ilani  kwa njia ya maandishi kuhusu uamuzi huo na pia atenge muda wa kumsikliza mwajiriwa huyo. Hata hivyo sehemu ya 42  ambayo inahusu mikataba hii ya majaribio ya kikazi ya waajiriwa inaeleza kuwa hayo hayatazingatiwa katika kuvunja mkataba kati ya mwajiri na mwajiriwa aliye kwenye majaribio ya kutathmini utendakazi wake. Dhima ya sehemu ya 42 ya sheria ya ajira yam waka wa 2007 ni kumruhusu  mwajiri kuweza kuuvunja mkataba huo kwa muda wowote iwapo hataridhishwa na utendakazi wa aliyemwajiri, sheria kwa hivyo inampa mwajiri uhuru wa kumweka mwajiriwa wake kwenye majaribio kwa miezi 12 na pia kuuvunja mkataba wao kwa ilani ya muda mfupi.
Katika kesi ya Danish Jalango na mwingine dhid yaAmicabre Travel Services [2014] eKLR. Walalamishi katika kesi hii walimshtaki mwajiri wao kwa kuwaachisha kazi kwa isiyo ya haki na kinyume na sheria , jambo lililokiuka mkataba wake wa kazi. Washtakiwa walitoa madai kuwa waliofutwa walikuwa wameajiriwa kwa mkataba wa majaribio ya kazi na hivyo hawakuwa na haki kwa mujibu wa sehemu ya 43  na 45 ya sheria ya ajira yam mwakawa 2007.
Mahakama ilishikilia kuwa mwajiriwa ambaye ako kwa mkataba wa majaribio ya utendakzi wake  kwa mujibu wa sehemu ya 42(2) ya sheria ya ajira  ya mwaka 2007 inaweza kuvunjwa bila kuzingatiwa kwa makadirio katika sehemu ya 43 na 45 ya sheria ya ajira .

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s