Sheria katika ukawaida wake inaeleza kuwa mwajiri ana wajibu wa kuwatunza wafanyikazi wao na kwa hivyo ana wajibu wa kuchukua hatua za kutosha ili kuhakikisha usalama wao wakiwa kazini. Katika kesi ya Efil Enterprises Limited dhidi Dickson Mathambyo Kilonzo [2018] eKLR. Mshtakiwa alikuwa amemwajiri mshtakiwa na siku hiyo ya tukio mwajiriwa akiwa anavuta toroli kwa kamba, Kamba iliyokuwa ikitumika ilikatika na kumsababisha kuanguka na kuumia. Mshtakiwa alikiri kuwa alichukua hatua ya kuvuta toroli ile kwa Kamba kwa sababu sehemu waliyokuwa wakipitia wakisafirisha mchanga na kokoto ilikuwa na mawe na miamba . Mlalamishi hakufanikiwa kuonyesha hatua yoyote ambayo aliichukua kuhahakisha kwamba mazingira ya utendakazi ni salama kwa wafanyikazi wake, hakukuwa na Ushahidi wa kuonyesha kuwa mshtakiwa alifanya jaribio lolote la kufanya njia ambayo mlalamishi angeitumia ili kuhakikisha kwamba mshtakiwa hatatakiwa kuivuta toroli ile.Rejelea tovuti:http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/162266/