Waajiriwa hawaruhusiwi kuwaajiri Watoto kwa ajira ambazo haziwafai. Kwa mujibu wa sehemu ya 53 ya sheria ya ajira, waajiri hawaruhusiwi kuwaajiri watoto katika ajira ambazo haziwafai. Sehemu hii pia inaeleza kuwa waziri wa leba anafaa kuweka vigezo ambavyo haviruhusiwi katika ajira . vigezo hivi vinaweza kuitangaza kazi, shughuli ama mkataba wa huduma kuwa mwovu kwa afya, usalama na maadili ya mtoto na kijisehemu (1) kitazingatiwa katika kazi na mikataba ya aina hiyo. Katika kesi Felister Nduku Nzaku dhidi ya Joyce Wairimu Gitau [2017] eKLR, katika kesi hii, mlalamishi alikuwa amajiriwa na mshtakiwa kama mjakazi akiwa na umri wa miaka 15. Mahakama ilibaini kuwa kumwajiri mtoto kama mjakazi wa nyumbani kunamnyima mtoto haki ya kupata matunzo na ulinzi, haki ya elimu na haki ya kufurahia Maisha yake ya utoto na mengine mengi ya kimsingi. Ajira kama hiyo ikiunganishwa na malipo dunia ma hata kutotoa malipo ya aina yoyote huo ukawa ukiukaji wa haki za mtoto maradufu. Rejelea tovuti: http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/144357