Sehemu ya 45 ya sheria za ajira inaeleza kuwa kuachishwa kazi kutakuwa kusiko kwa haki iwapo mwajiri atashindwa kuthibitisha kuwa ana sababu yenye mashiko kihaki ya kumwachisha kazi mwajiriwa , sababu itakuwa ya haki iwapo itaweza kuonyesha kuwa kuna uhusiano kwa tabia ya mwajiriwa , uwezo wake wa kutenda kazi , uwezo wake wa kuafikia viwango vya utendakazi anvyovitaka mwajiri wao na iwapo kuachishwa kwao kazi kulifuata utaratibu unaohitajika. Mtu anweza tu kudai fidia isiyo ya haki iwapo atakuwa amemfanyia mwajiri wake kazi kwa miezi 13 mtawalia. Katika kesi ya Gilbert Mariera Makori dhidi ya Benki kuu ya Equity (2016) eKLR. Mahakama katika kesi hii iliripoti kuwa : sehemu ya 41 ni muhimu sana katika utaratibu utakaofuatwa kabla ya mwajiriwa kufutwa kazi kwa misingi ya tabia , matokeo duni kazini ama ulemavu., mwanzo ni lazima mwajiri amwelezee mwajiriwa kwa lugha anayoielewa sababu ya kutaka kumfuta kazi , hili linafaa kufanyika mbele ya mwajiriwa mwenza atayemchagua huyu anayeachishwa kazi ambaye pia anaweza kuwa afisa wa muungano wa wafanyikazi. Baada ya maelezo hayo mwajiri atazingatia maelezo ya mwajiri wake au yale ya wawakilishi wake kabla ya kuafanya uamuzi wa iwapo atamwachisha mwajiri wake kazi au la. Rejelea tovuti: http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/128282