Mwajiri ana wajibu wa kudumisha imani na uaminifu kwa waajiriwa wake. Sheria katika ukawaida wake inaeleza kuwa mwajiri bila sababu yoyote hafai kuhusiana ana waajiriwa wake kw njia ambayo inaweza kudhuru uhusiano wake na wajiriwa wake. Katika kesi ya Lawrence Onyango Oduori dhidi ya benki kuu ya Commercial, mlalamishi aliwasilisha kesi mahakamani dhidi ya mwajiri wake ambaye ni Benki kuu ya Kenya. Alidai kuwa alikuwa ameachishwa kazi kwa njia isiyo ya haki, alidai kuwa alikuwa ameachishwa kzi bila utaratibu unaofaa kuzingatiwa, alishuku uhalali wa sababu iliyotolewa katika kutetea kuachishwa kwake kazi pamoja na usawa uliokuwa katika utaratibu uliotumiwa kumtimua.Katika kesi hii Mahakam iliongezea kuwa, “uhusiano wa ajira umejengwa katika misingi ya Imani na uaminifu. Mpito mrefu wa wakati unahujumu uwezekano wa Imani hiyo kujengeka tena. Rejelea tovuti: http://kenyalaw.org/caselaw/cases/view/98288/