Sehemu ya 6 ya sheria ya ajira inapiga marufuku vikali kila aina ya dhuluma za kingono katika mazingira ya kazi. Kwa mfano katika kesi ya Vishaka na Ors katika Mahakama ya Upeo ya India dhidi ya jimbo la Rajasthan na Ors (J), 1997 (7) SC 384). Jaji alibaini kuwa ni jukumu la mwajiri au watu wengine waliowajibika katika sehemu za kazi kuzuia vitendo vyovyote vya dhuluma ya kingono na kutoa mikakati ya kupinga na kushtaki vitendo vyovyote vya dhuluma ya kingono. Rejelea tovuti: https://indiankanoon.org/doc/1031794/