Mwajiri ana wajibu wa kupiga ripoti kwa afisa anayesimamia afya na usalama wa waajiriwa ndani ya siku saba baada ya kutokea kwa jeraha.

Sehemu ya 21 (3) ya sheria ya afya na usalama katika sehemu za makazi inaeleza kuwa: mahali ambapo ajali katika sehemu za inasababisha majeraha ambayo hayaleta kifo cha mwathiriwa , mwajiri anafaa atume ujumbe kwa njia ya maandishi kuhusu tukio hilo ndani ya siku saba baada ya kutokea kwa tukio hilo. Katika kesi ya Julius Chacha Mwita dhidi ya kampuni ya uchukuzi kwa ndege  Kenya Airways na mwinginee( 2015) eKLR , mahakami ilibaini kuwa mwajiri alikuwa amekosa kuwasilisha ujumbe kuhusu tukio la  jeraha kwa mlalamishi mnamo mwaka wa 2010, na sasa ilikuwa mwaka wa 2012 wakati ambapo ujumbe ukitumwa kwa mkurugenzi, kwa sababu hiyo mahakama ilidumisha sehemu ya 21(3) inayosema kuwa ujumbe huo ni sharti utmwe ndani ya siku saba kutokea siku ya tukio la jeraha. Rejelea tovuti: http:/kenyalaw.org/caselaw/cases/view/112319

Leave a comment