vidokezo vya sheria za Leba

Kujifunza na elimu ni safari. Ni mchakato unaoendelea wa muda mrefu. Elimu ndio inayowezesha uendelevu wa uchumi wa jamii na wa nchi kwa jumla.

Jifunze ‘kitu kimoja’ kila siku kutoka kwa chanzo cha kuaminika cha waalimu, watendaji na washauri katika sheria na uzoefu wa zaidi ya miaka 20. Mwaka huu, SheriaTips imeshirikiana na Haki Mashinani ili kuelimisha na kuwezesha waajiri na wafanyikazi na waajiri juu ya haki zao na majukumu mbali kama Sheria ya Kazi inavyotuelekeza. Kupitia teknolojia, Sheriatips iliunda jukwaa ambalo linaweza kutuma ujumbe mfupi, bila malipo, juu ya maswala yanayohusu haki za kazi, unyanyasaji wa kijinsia katika sehemu za ajira kati ya mada zingine. Mpokeaji baada ya kupokea ujumbe mfupi anaweza kuchagua kusoma yaliyomo zaidi ya ujumbe huo na hata kupata msaada wa kisheria kwa kutuma ujumbe wa pepe kupitia ukurasa huu ili kuelekezwa kwa NGO na wasaidizi wanasheria ambao wanasaidia bila malipo, na wanaojulikana kama ‘pro bono’ lawyers.

 1. Angalia Maudhui mbali mbali kuhusu sheria za leba
 2. Haki ya mwajiri kukata ujira kwa kiasi kifaacho kisheria
 3. Haki ya mwajiri kukata ujira kwa siku ambazo kazi haijafanyika 
 4. Haki ya waajiri kukata hela zifaazo kwa uharibifu wa mwajiriwa
 5. Mwajiri ana wajibu wa kukata kiwango cha hela zinzohitajika katika akiba za kimsingi za mwajiriwa.
 6. Wajiri wana haki ya kutoa taarifa kwa waajiriwa wao kuhusu sheria za kazini pamoja na adhabu yake.
 7. Jukumu la waairiwa kuwajibikia hela zilizo chini ya utunzi wao
 8. Haki ya kutarajia umakini na uangalifu pamoja na matumizi ya maarifa kutoka kwa waajiriwa.
 9. Haki ya kutarajia umakini na uangalifu pamoja na matumizi ya maarifa kutoka kwa waajiriwa.
 10. Uhuru wa Mwajiri kushiriki na shughuli za vikundi vya waajiri
 11. Mwajiriwa anafaa kutii maagizo ya kazini 
 12. Mwajiriwa anafaa kufuata sheria kabla ya kujiuzulu kazini.
 13. Mwajiri lazima kufuata sheria anapomtimua mwajiriwa kazini.
 14.  Wajibu wa mwajiriwa kutuma mavazi yafaayo kazini.
 15. Jukumu ya mwajiri kuhakikisha usalama na afya bora kazini.
 16. Haki ya mwajiri kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya mwajiriwa.
 17. Haki ya mwajiri kukagua utendakazi wa mwajiriwa.  Haki ya mwajiriwa kulipwa mshahara wa mwezi mmoja anapoachishwa kazi.
 18. Haki ya mwajiri kumshusha mwajiriwa wake cheo kazini.
 19. Haki ya mwajiri kumpandisha mwajiriwa wake cheo.
 20. Haki ya mwajiri kuwataka waajiriwa kuwa waaminifu, waadilifu na wenye imani kwa mwajiri wao.
 21. Jukumu la mwajiriwa kutoingilia biashara ambayo ina ushindani na ile ya mwajiri wake.
 22. Wajibu wa mwajiri kuifadhi rekodi za waajiri wake.
 23. Haki ya mwajiri kushiriki uchaguzi katika vikundi vya waajiri
 24. Haki ya mwajiri kujuzwa mwajiriwa anapoondoka kwenda likizo
 25. Haki ya waajiriwa wa jinsia ya kike kwenda likizo ya uzazi
 26. Jukumu la kuwajuza waajiri kuhusu majeraha katika kazi
 27. Jukumu ya mwajiri kuhakikisha usalama na afya bora kazini.
 28. Haki ya mwajiri kutayarisha mkataba wa ajira
 29. Jukumu la waajiriwa kuifadhi siri za kazini.
 30. Mwajiriwa anafaa kufuata sheria kabla ya kujiuzulu kazini. 
 31. Haki ya mwajiri kujuzwa kuhusu matibabu
 32.  Mwajiriwa anaweza tu kutimuliwa kazini kwa njia ya maandishi kwa mujibu wa sheria.
 33. Mwajiriwa anafaa kufuata sheria kabla ya kujiuzulu kazini.
 34. Mwajiri ana wajibu wa kutayarisha mkataba wa ajira unaoratibu yote ya kimsingi kuhusu ajira.
 35. Haki ya mwajiri kumfuta kazi mwajiriwa bila ilani kwa mujibu wa sheria.
 36. Mwajiri ana wajibu wa kutoa/kuwasilisha msimamao wake/ wa shirika kuhusu suala la unyanyasaji wa kijinsia.
 37. Mwajiri ana haki ya kuchukua hatua za kuwahakikishia haki wanaochukuliwa kuwa wanyonge.
 38. Ni hitaji la sheri kwamba kandarazi ya huduma iwe katika maandishi.
 39. Waajiri wana haki ya kuajiri kwa mujibu wa utaratibu uliopo wa kitaifa wa kuajiri.
 40. Mwajiri ana haki ya kuwatenga waajiriwa kufikia baadhi ya vitengo vya ajira .
 41. Kila mmoja ana haki ya usawa katika utekelezaji wa kazi yake.
 42. Waajiriwa wana haki ya kupata ujira sawa kwa kufanya kazi ya thamani sawa.
 43. Waajiriwa ambao utendakazi wao haujadumu kwa muda wa zaidi ya miezi mitatu hawana haki ya kupatiwa mkataba wa ajira ulioandikwa.
 44. Mwajiri ana wajibu wa kuandika/ kutengeneza kandarasi ya ajira.
 45. Mwajiriwa ana haki ya kukubaliana na vigezo na masharti ya ajira kwenye mkataba.
 46. Mwajiri ana haki ya kusalia na hifadhi ya stakabadhi za mwajiriwa hata baada ya kumwachisha mwajiriwa kazi.
 47. Kandarasi ya ajira huongozwa na sheria za utendakazi (leba) kabla ya sheria za kawaida za mikataba.
 48. Waajiri wana haki ya kudhibiti masaa ya kufanya kazi mradi wawalipe waajiri kwa masaa wanayofanya kazi
 49. Sheria inaruhusu kuachishwa kazi bila ilani kwa wafanyikazi ambao hufanya kazi na kulipwa kila siku.
 50. Waajiriwa wana wajibu wa kutii na kuzingatia utaratibu wote wa afya na usalama unaowekwa na mwajiri.
 51. Waajiri waripoti matukio yoyote ya hatari kule kazini kwa wakubwa/wasimamizi wao.
 52. Mwajiriwa anapaswa kuripoti ajali katika sehemu za kazi.
 53. Mwajiriwa ambaye amepata jeraha akiwa angali kazini ana haki ya kupewa fidia isipokuwa iwapo jeraha hilo lilitokea kutokana na ukosefu wake wa uangalifu.
 54. Mwajiriwa ana jukumu la kukubali kupokea matibabu kusudi jeraha lisiwe baya Zaidi.
 55. Haki ya kupata fidia inakamilika baada ya miezi kumi na miwili baada ya kutokea kwa ajali.
 56. Mwajiriwa ana wajibu wa kupeana ilani iwapo amepatwa na maradhi yanayotokana ana kazi anayoifanya mwajiriwa haraka iwekanavyo na katika maandishi.
 57. Mwajiriwa ana wajibu wa kuwatunza waajiriwa wenza
 58. Haki ya mwajiriwa kutambua muungano wa waajiri
 59. Haki ya mwajiriwa kujiunga na muungano wa wafanyikazi
 60. Haki ya mwajiriwa kujiuzulu kutoka kwa ajira yake.
 61. Haki ya mwajiriwa kupata likizo ya kila mwaka.
 62. Haki ya mwajiri kumwondoa mwajiriwa kazini kwa ajili ya kupunguza gharama ya utendakazi
 63. Haki ya kulipwa malipo sawa na kazi inayofanywa
 64. Haki ya mwajiriwa wa kiume kupewa likizo fupi ya uzazi.
 65. Haki ya mwajiriwa kuvunja mkataba wa majaribio ya utendakazi wake bila ilani yoyote au ilani ya muda mfupi.
 66. Wajibu wa mwajiri kumueleza mwajiriwa sababu ya kufutwa kazi.
 67. Haki ya mwajiriwa kutobaguliwa kwa kazi
 68. Mwajiri ana wajibu kuhakikisha kuwa waajiriwa wake wana mazingira salama na safi ya kufanyia kazi.
 69. Waajiriwa hawaruhusiwi kuwaajiri Watoto kwa ajira ambazo haziwafai.
 70. Waajiriwa wana haki ya kutoachishwa kazi kwa njia isiyo ya haki.
 71. Mwajiri ana wajibu wa kuwapa waajiwa wake vifaa/mavazi ya kujikinga dhidi ya madhara yoyote wakiwa kazini
 72. Kila mwajiri ana haki ya kuhahaikisha kuwa mazingira zake za utendakazi ni salama kwa wajiriwa wake.
 73. Mwajiri ana haki ya kususia kazi ambayo inayatia maisha yake hatarini. 
 74. Haki ya mwajiriwa kuchukua mikakati inayofaa ili kuhakikisha yuko salama akiwa kazini.
 75. Wajibu wa mwajiri kudumisha imani na uaminifu kwa waajiriwa wake.
 76. Kila mwajiri ana haki ya kupata siku moja ya mapumziko katika juma
 77. Mwajiri ana wajibu wa kupiga ripoti kwa afisa anayesimamia afya na usalama wa waajiriwa ndani ya siku saba baada ya kutokea kwa jeraha.
 78. Tukio la ajali katika sehemu ya kazi linaweza kuwasilishwa kwa mwajiri ka njia ya mdomo.
 79. Mwajiri an wajibu wa kuhakikisha kuwa dhuluma za kingono hazijafanyika katika sehemu za kazi.

Wasiliana nasi!